0


⁠⁠⁠Na Agness Francis, Globu ya Jamii 

Mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF),Iman Omary Madega amesema atashirikiana na klabu za soka kwa ajili ya kuleta maendeleo ya soka ya nchini pamoja na kuhakikisha wanapatikana wadhamini watakaosaidia maendeleo zaidi.

Madega ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea, pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga amenadi sera zake leo Jijini Dar es salaam  kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 Mkoani Dodoma.

 Akinadi Sera zake ambazo zinalenga hasa katika uadilifu,utendaji na uwazi amesema kuwa atakuwa bega kwa bega na klabu zote bila kubagua endapo atachaguliwa kuwa Rais wa shirikisho la kabumbu nchini kuachilia mbali kuwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga mwaka 2005-2010 chini ya uongozi wa Leodger Tenga na kuwataka wapenda soka kuondoa shaka kwa hilo.

 Madega amesema ili kuweza kuongoza vizuri tasnia hii ya soka inaitaji muda ili kufanikisha utendaji mzuri wa kazi na kupiga hatua mbele zaidi katika soka.

 Mgombea huyo amesema lengo lake ataakikisha analeta mafanikio katikan sekta ya soka nchini kwa kuwapandisha Tanzania kutoka viwango vya sasa 120 vilivyopo kwa sasa na kushuka zaidi chini ili kuwa katika viwango bora duniani.

Katika soka la wanawake, Madega amehakikisha kuwa atatenga bajeti ya kutosha itokanayo na wadhamini ili waweze kucheza soka la mikoa yote nchini ili kukuza vipaji zaidi na ili kuwa na maendeleo hayo na kufikia hatua ya kimataifa atahakikisha anaboresha mahusiano mazuri kati ya TFf na serikali yetu,kuboresha viwanja vya mpira nchini, pamoja makocha wazuri na waamuzi wenye uwezo mkubwa wa kuchezesha mechi za kimataifa.

 Madega ametoa wito kwa wapiga kura kumchagua kuwa kinara katika uchaguzi huo wa shirikisho La soka Tanzania (TFF) utakaofanyika tarehe 12 agosti mwaka huu mjini Dodoma.

Post a Comment

 
Top