Wadau wa maendeleo wilaya ya Kilwa,mkoani Lindi,wameishauri Serikali mitaala ya kodi kufikisha hadi kwenye Shule za msingi na Sekondari,kwa lengo la kuwajengea wanafunzi kuwa raia wema waweze kuwa na utamaduni wa kulipa kodi hapo baadae.
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo, kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa Asasi za kijamii na wawakilishi wa Chama cha walimu (CWT) juu ya umuhimu wa huduma ya elimu na ukusanyaji mapato ya Serikali, yanayofanyika mji mdogo wa Masoko juma lilopita mwezi huu juni.
Post a Comment