0


Leo Jumapili ya June 11 2017 michuano ya SportPesa Super Cup yaliyokuwa yanashirikisha timu nane, kati ya hizo nne kutoka Kenya na nyingine kutoka Tanzania yamemalizika rasmi kwa kuchezwa mchezo wa fainali ya michuano hiyo kati ya AFC Leopards dhidi ya Gor Mahia.

Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kama kawaida imechezwa katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, mchezo kati ya AFC Leopards dhidi ya Gor Mahia huwa ni mchezo ambao una upinzania mkubwa sana nchini Kenya na unajulikana kwa jina la Mashemeji Derby.
Gor Mahia ambao walionekana kuwa na mashabiki wengi katika game ya leo kuliko AFC Leopards wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0 ambao yamewafanya kuwa Mabingwa wa SportPesa Super Cup 2017, magoli ambayo yalifungwa na Timothy Otieno dakika ya 60, Oliver Maloba dakika ya 71 na Ndirangu John dakika za nyongeza.
Ushindi huo sasa unaipa nafasi Gor Mahia ya Kenya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Everton ya England ambao watakuja kucheza na Bingwa wa SportPesa Super Cup July 13 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, kama utakuwa unakumbuka vizuri michuano hii ilishirikisha timu za Simba, Yanga, Singida United, Jang’ombe Boys, AFC Leopards, Gor Mahia, Nakuru All Stars na Tusker FC.

Post a Comment

 
Top