0
 Image result for MATATIZO YA LAPTOP
Kwa leo tutazungumzia tatizo lifuatalo;

4. BETRI KUSHINDWA KUPATA MOTO (KUCHARGE).
Tatizo hili hutokea katika hali mbalimbali kutokana na chanzo cha tatizo hilo ambalo limetokea kwenye Kompyuta yako.
(i) Kompyuta kuzima pale Charger (Adapter) inapotolewa kwenye Kompyuta.
Na ukipeleka “cursor” kwenye sehemu inayoonesha betrii utakuta inakuonesha “100% charging” lakini baada ya hapo ukitoa “Adapter” Kompyuta yako inazima, hii inaweza kusababishwa na mambo haya.
(a) Betri haijawekwa vizuri kwenye Kompyuta yako.
(b) Betri limepata Kutu, hii ikiwa na maana kuwa inashindwa kufanya mawasiliano vizuri na Ubao Mama(Motherboard). Hapa safisha betri lako kwa kutumia “electronic cleaner” sehemu ambayo ndiyo kiunganishi cha betri yako.
(c) Ukiona umesafisha vizuri lakini tatizo limebaki kuwa hilo hebu badilisha betri lako.
(d) Ukibadilisha betri nab ado tatizo likabaki kuwa kama lilivyo hapo tatizo litakuwa kwenye Ubao Mama(Motherboard), hivyo unaweza kutengeneza Motherboard au Ukabadilisaha Motherboard nzima kutatua tatizo.

(ii) Betri kutoonesha kuchaji (The battery not detected).
Sababu za kutokea tatizo hili inaweza kuwa
(a) Betri ni bovu, linatakiwa kubadilishwa.
(b) Ukibadilisha bado tatizo likabaki kuwa hivyo, hapa Lazima Motherboard itakuwa imepata hitilafu, hivyo
 unaweza kuitengeneza au kuibadilisha.

(iii) Betri inaonesha imajaa kabisa 100% baada ya Muda mfupi inapungua mpaka 80% baadaye kidogo inapungua hadi 0%, Ukiona hivyo jua kuwa tatizo ni Betri linashindwa kufanya vyema, hivyo ni bora ukanunua betri mpya.
(iv) Betri inapokuwa inacharge pale “Adapter” inapowekwa sehemu sahihi, uonapo hivyo fahamu kuwa inawezekana lipo tatizo kwenye;
(a) Charger (Adapter) imekufa. Hapa angalia Power cable, au Adapter yenyewe, kimeojawapo kinaweza kuwa kimepata hitilafu.
(b) Kama Adapter inafanya kazi vizuri, yawezekana tatizo lipo kwenye “Power jack” (connector where you plug power adapter- charging system). Hapa suluhisho lake ni kuibadilisha.



1.. KIBODI (KEYBOARD):
Kibodi inatumika kwa ajili ya kuingizia herufi, namba, alama na michoro, nayo imegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni kama ifuatavyo: Funguo za kuandikia (Typewriter keys), funguo za kuhama (Movement keys), funguo za namba pamoja na michoro mingine (Numeric keys) na funguo za kazi ( Function keys)
Kibodi ni muhimu sana kwa ajili ya matumizi ya Kompyuta maana ndipo tunapopata maandishi mbalimbali kama ilivyoelezwa hapo juu pale unapokuwa unaandika habari mbalimbali kwenye Kompyuta yako.

MAMBO YANAYOSABABISHA KUHARIBIKA KWA KIBODI(Keyboard).
Mambo haya yamegawanyika katika vipengele vifuatavyo;

1.Kuacha Kompyuta muda mrefu bila kutumika,
  Tatizo hili linatokea pale Kompyuta unapokuwa umeiacha muda mrefu, ambapo wakati unaacha kuitumia yawezekana ilikuwa na vimiminika/unyevunyevu, kitendo ambacho hupelekea vimiminika hivyo kujikusanya pamoja na kutengeneza kitu kama kutu, mwishowe husababisha kupitisha “signal” kwa kiwango hafifu, au kuharibika kabisa.
2. Kumwagiwa kimiminika kwenye kibodi hiyo, kama chai, uji, soda n.k. Vimiminika hivi vimekuwa chanzo cha kuharibu kibodi.

DALILI ZA KUHARIBIKA.
Hizi ni dalili mbalimbali ambazo hutokea pale kibodi inapoharibika;

1. Funguo/key kuandika herufi Zaidi ya moja, mfano badala ya kuandika “U” huandika “T”, “N” “3” n.k.
2. Kuchelewa kuhisi (ku-sense) mfano unabonyeza herufi M inajitokeza baada ya Sekunde kadhaa.
3. Kutofanya kazi kabisa kwa kibodi.

JINSI YA KUTATUA TATIZO LA KIBODI.
1. Safisha kibodi yako kwa kitambaa kikavu huku ukitumia “isopropyl alcohol” hii husafisha kibodi na kukaa katika hali nzuri, na pia unaweza kuitumia kusafisha Kompyuta yako.
2. Kubadilisha kibodi(keyboard), ubadilishaji huo huendana na model/aina ya Kompyuta yako. Hakikisha unaangalia “model” ya Kompyuta yako ili upate keyboard inayoendana na Kompyuta yako.


MATATIZO YANAYOIKUMBA KOMPYUTA, PAMOJA NA SULUHISHO LAKE.

2. KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA (MOTHER BOARD)
Ubao Mama(Motherboard), hii ni Saketi ambayo ina muunganiko wa “chip” Zaidi ya moja. Inaitwa Saketi kwa sababu inatumia umeme wa moja kwa moja (Direct Current).
Kwanini uitwe Ubao mama(Motherboard)? Kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuweza ku-programu(programing). Ina uwezo mkubwa wa kutoa kitu toka kwenye “electronic” kwenda kwenye “electronic software”.
Kwa kawaida Ubao mama unapatikana kwenye Kompyuta hapa nikiwa na maana kwenye Simu, radio, Tv, Laptop, Desktop, Mackbook n.k., maana hivi vyote viko kwenye mfumo mzima wa Kompyuta.
Lakini sisi kwa leo tutajikita kwenye Ubao mama (motherboard) kwenye Laptop pamoja na Desktop.
DALILI za kuharibika kwa ubao mama, hii ni hali ambayo hutokea ambapo Kompyuta ilikuwa inawaka lakini ghafla Kompyuta huzima na kuacha kuwaka kabisa.
    
SABABU(VISABABISHI) ZA KUHARIBIKA UBAO MAMA.
1. Kuchemka/ kupata joto jingi kwa Kompyuta, jambo ambalo husababishwa na Kushindwa kufanya kazi kwa feni(fan).
2. Kumwagiwa kimiminika(liquid), kwenye Kompyuta, pale Kompyuta inapomwagiwa vitu kama chai, soda, maji, uji, n.k huweza kusababisha kuharibika kwa motherboard.
3. Kuwepo kwa uchafu, moshi, kwenye Ubao mama(motherboard), kama Kompyuta haifanyiwi usafi pia inaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa ubao mama.
4. Kuanguka kwa Kompyuta, kuvunjika.
5. Umeme kuzidi kwenye Kompyuta.
6. Kutumika kwa Muda mrefu(kuzeeka).

JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI LA KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA(MOTHERBOARD).
1. Utatuzi wa Shida(troubleshooting),
(i) Angalia kama kuna “signal” zinazoonesha kama umeme unaingia kwenye Motherboard, hapa angalia kwenye “Power jeck” kama umeme unaingia kwenye motherboard.
(ii) Pima “component” mbalimbali zinazounda mfumo mzima wa ubao mama, moja baada ya nyingine kwa kutumia kifaa kinachoitwa “Multimeter, ukigundua “component” ambayo ni mbovu waweza kuibadilisha.
Kabla ya kuibadilisha hiyo “Component” yafaa ukaangalia vitu vifuatavyo;
- Uthamani/ufanano wa “component” unazotaka kubadilisha.
- Utendaji wa kazi wa “component” hiyo.
(iii) Kuibadilisha “component” hiyo. Hapa utaamua kuibadilisha component hiyo kwa kuweka “component” nyingine ambayo ni nzima kama ilivyokuwa mwanzoni.
(iv) Fanya usafi kwenye Ubao mama(Motherboard) pamoja na Kompyuta nzima kwa ujumla.
(v) Washa Kompyuta yako.
2. Kubadilisha Ubao Mama (Ubao Mama), wakati mwingine Unaweza ukabadilisha “Component” lakini bado tatizo likabaki palepale au ukakosa “component” za kubadilisha kwenye ubao mama na zile zilizoharibika, hivyo lazima ubadilishe ubao mama huo kuendana na “MODEL” ya hiyo Kompyuta yako.
TAHADHARI: Usithubutu kufungua kama wewe sio “technician”/fundi maana unaweza kusababisha matatizo mengine pia.

 KUPATA JOTO KWA KOMPYUTA (COMPUTER OVER HEATING- PROCESSOR).
Kompyuta kupata joto ni muongezeko wa joto kwenye mfumo mzima wa utendaji wa Kompyuta kwa ujumla.
Hili tatizo kwa kawaida husababisha na mambo mbalimbali ambayo ni;
1. Kuwepo kwa uchafu kwenye “Cooling system”, hii mara nyingi hutokea pale ambapo unakuta mtumiaji hana mazoea ya kufanya service kwenye Kompyuta yake ili kuondoa baadhi ya uchafu ambao unaweza kuwa chazo cha kuzuia Feni isiweze kufanya kazi kwa umaridadi mkubwa na kupelekea mfumo wa utendaji (Operating system) kufanya kazi.
2. Kuyeyuka kwa “Thermal compound”.  Hii thermal compound ambayo ni hukaa kati ya “processor” pamoja na “sink” ikiyeyuka na kupoteza ubora wa kusafirisha joto/temperature vizuri na kwa utaratibu, jambo ambalo husababisha kuongezeka kwa joto n ahata kusabisha kusambaa maeneo mengine ya Kompyuta.
3. Kuharibika kwa Feni, Kwenye mfumo huu mzima wa “Cooling” feni inasimama kama kipozeo, hivyo feni ikiharibika uwepo wa joto unakuwa mkubwa sana.
Dalili za Tatizo hili la Kuongezeka kwa joto kwenye Kompyuta.
1. Uendeshaji wa Mfumo wa Utendaji wa Kompyuta (Operating system) hupungua.
Hapa ndipo unakutana na kupungua kwa kasi/speed ya Kompyuta, na hasa unapokuwa upo kwenye maatumizi ya intanet inakuwa vigumu sana katika kufanya kazi zako.
2. Joto jingi sana kwenye Kompyuta yako, ukiishika Kompyuta yako utahisi imechemshwa kwenye moto.

Madhara yatokanayo na Kuongezeka kwa joto kwenye Kompyuta.
1. Kompyuta kuzima, mara nyingi Kompyuta inaweza kuzima ghafla na isiweze kuwaka tena.
2. Kuungua kwa Kompyuta, joto likizidi kwenye “cooling system” linaweza kusambaa sehemu zingine za Kompyuta n ahata Kompyuta nzima, kitendo ambacho moto unaweza kuunguza hata baadhi ya “chip” ambazo ni muhimu sana katika mfumo mzima wa Kompyuta na mwishowe hupelekea Kompyuta kuungua kabisa.\

Jinsi ya kutatua tatizo la Kuongezeka kwa joto kwenye Kompyuta.
1. Kusafisha feni mara kwa mara, hapa nazungumzia usafi kwenye feni ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi na kiwango cha hali ya juu.
2. Kuangalia feni kama inafanya kazi kwa kiwango cha kawaida ambacho ni rafiki kwenye utendaji mzima wa “cooling system”.
3. Kubadilisha feni, utafikia uamuzi huo baada ya kuangalia kama feni yako ni mbovu na kluweka feni nyingine ambayo ni nzima.
N.B Feni hizi pia hutofautiana kutokana na model ya Kompyuta yako. Hivyo ukitaka kuibadilisha feni yako hakikisha “model” zinafanana.

Katika kutengeneza “Cooling system” fuata hatua hizi za kiufundi.
1. Zima Kompyuta yako kama itakuwa imewashwa
2. Ondoa betri.
3. Ondoa “charger adapter”.
4. Sasa unaweza kufungua Kompyuta yako na kusafisha “Cooling sytem” ili kuondoa uchafu wote unauzuia utendaji mzima wa “Cooling system”.

Post a Comment

 
Top