0
Baadhi ya wanawake wilayani Liwale mkoani Lindi wakinyanyua juu keki ni ishara ya upendo,umoja n a ushirikiano kwenye jamii hivyo uleta maendeleo
Kwenye hafla hiyo mgeni rasmi ni Bi Sarah Chiwamba aliyekaa katikati ambaye ni mkuu wa wilaya ya Liwale

  Bi Sarah Chiwamba akizungumza na wanawake huku akisisitiza watu watumishe amani 
Wanawake wilayani Liwale mkoani Lindi wametakiwa kuthubutu na kujiamini kwenye utendaji wao wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa lengo la  kuufikia uchumi wa viwanda.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Liwale Bi Sarah Chiwamba kwenye hafla maalum ya wanawake iliyofanyika Usiku wa March 10 kuamkia March 11, 2018 katika ukumbi wa Tengeneza Liwale Mjini ambapo amsema kuwa wanawake wakithubutu na kujiamini wataweza kuufikia uchumi wa viwanda kwa kasi hitajika
   
Mkuu wa wilaya Chiwamba amewahakikishia wanawake wa wilaya ya Liwale kupatiwa mikopo yenye tija  inayotokana na makusanyo ya ndani ya Halmashauri hiyo bila ya kuwa na pingamizi lolote kutoka kwa mtu yeyote kwani hilo ni hitaji la kisheria na halina uhiari katika utekelezaji wake


Awali kwenye hafla hiyo wanawake hao waliweza kuchagua wanawake wanaojituma katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo ambao wamekuwa mfano katika jamii kwa mwaka wa 2017/2018 ambapo wanawake wawili wamechaguliwa kuwa mzuri wa kuigwa ambao ni Bi Somoe Ngatumbula  (kushoto pichani) na Mwalimu Somoe Ukomo (kulia pichani) na  wanaeleza jinsi walivyopata nafasi hiyo.
 Bi Ngatumbula
  Bi. Ukomo 
"Jitihada na kujituma ndio siri ya mafanyikio ya haya yote na pale unaoona umekwama unatakiwa kuomba msaada wa mawazo ili kuweza kupata ufumbuzi wa kile ulichokwama pia walisema ukichukua mkopo tumia kwa malengo" walisema mabi Ngatumbula na Ukomo 

Liwale Blog na Mashujaa fm 89.5 iliyokuwepo hapo muda wote huo ili kushuhudia kile kinachoendelea kwenye ukumbi huo mwishoni mwa hafla hiyo imeweza kuzungumza Mwanadada Saida aliyetumia nafasi hiyo kuelezea nafasi hizo za kuwatambua wanawake hao kama ni watu wa mfano wa kuigwa kwenye jamii na hapa anaelezea zaidi.

Hafla ya Wanawake hawa inafanyika ikiwa ni Siku chache tangu Wanawake wote Nchini waungane na wenzao Ulimwenguni kote kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika March 08,Mwaka huu ambapo kwa Wilaya ya Liwale shughuri hiyo kiwilaya ilifanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri na Mh.Amida Abdallah ndiye aliyekuwa mgeni wa Heshima Siku hiyo.
       Hapa ni sehemu ya burudani kila mtu alionyesha uwezo wa kucheza 

Post a Comment

 
Top