Wajumbe wa bodi ya Chelsea wameonyesha kukasirishwa na uamuzi wa Kocha Antonio Conte kuchukua uamuzi wa kumuambia mshambulizi wake, Diego Costa kwamba hatakiwi.
Conte alimuambia Costa hatakiwi kwa ujumbe mfupi wa simu au SMS, jambo ambalo limewashangaza na kuwakasirisha mabosi hao.
Awali ilielezwa kwamba huenda Conte akawa matatizoni na kuingia kwenye hofu ya maendeleo yake ndani ya klabu hiyo. Hata hivyo lazima atahojiwa kuhusiana na uamuzi wake huo ambao umeonekana si wa kiungwana kwa Costa.
Lakini taarifa nyingine zinaeleza, kuna hofu ya kumuacha Conte kwa kuwa watawaudhi mashabiki.
Imani ya Conte kwa mashabiki wa Chelsea iko juu sana kutokana na mabadiliko na alivyoweza kuituliza timu kwa kipindi kifupi.
Post a Comment