Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imetoa hukumu ya
kurejeshwa nchini kwao Raia watatu wa Pakistani waliokuwa wakiishi hapa
nchini Tanzania kufuatia kukutwa na hatia ya makosa mbalimbali ikiwemo kosa la
kuhujumu mitambo ya mawasiliano ya Kimataifa na kuisababishia serikali
hasara ya mamilioni ya pesa kupitia mamlaka ya mawasiliano Tanzania
TCRA.
Raia hao wa kigeni ni Hafeez Irfan, Mirza Irfan Baig na Mirza Riwan Baig ambapo inatajwa kuwa mnamo october 15 mwaka jana wakiwa katika hotel ya Buterfly iliyopo Kariakoo jijini Dar es salaam walifanya kosa hilo kwa kutumia vifaa maalum vya mawasiliano vilivyotumika kupiga simu za kimataifa pasipo kibali maalum cha Mamlaka ya Mawasiliano nchini ambapo watuhumiwa hao walikiri kutenda makosa hayo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Respicius Mwijage amesema kwa Mujibu wa sheria za jamuhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa hao watalazimika kulipa faini ya shilingi milioni 40 kwa kila mmoja au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela sanjari na kurejea nchini kwao mara moja pindi watakapokamilisha taratibu za ulipaji faini.
Akizungumzia hukumu hiyo Mwanasheria wa Mamlaka ya mawasiliano Nchini TCRA JOHANNE KALUNGURA ameeleza kuridhishwa na adhabu iliyotolewa na Mahakama na kuongeza kuwa itakuwa fundisho kwa wenye nia ovu ya kuhujumu Uchumi wa nchi.
Katika hatua nyingine Mahakama hiyo imewasomea mashataka Raia 7 wakiwemo watanzania na wa mataifa mengine wanaodaiwa kuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kwa kufanya kosa la matumizi mabaya ya mitandao wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana na kesi yao kutajwa tena Decemba 1 mwaka huu.

Post a Comment