Serikali imekemea tabia ya baadhi ya watumishi wake wanaoshindwa
kuwajibika ipasavyo katika majukumu yao, lakini wakiwa nje ya serikali
ama kwa kupitia makampuni binafsi wanayomiliki wanafanya vizuri na kwa
ufanisi mkubwa.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametoa karipio hilo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua kongamano na mkutano mkuu wa Chama chama cha wapima ardhi Tanzania IST, na kubainisha kuwa migogoro mingi ya ardhi ukiwemo ujenzi holela vimesababishwa uwajibikaji mbovu wa baadhi ya watumishi waliopewa dhamana.
Amesema kutokana na mwamko wa wananchi kutaka huduma ya kupima maeneo yao ya ardhi, wapima ardhi hawana budi kutekeleza wajibu huo kwa umakini mkubwa, maarifa ya kitaalam, teknolojia na nguvu za ziada ili kuwezesha mipango ya uwekezaji katika ardhi inafanikiwa.
Awali Rais wa IST Bw. Martins Luther Chodota alieleza mipango mbalimbali ya chama hicho kushirikiana na serikali kutekeleza majukumu yake kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa, hatua ambayo itasaidia eneo kubwa la nchi kupimwa, na hatimaye kupunguza migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiongezeka, ikiwemo ya wakulima na wafugaji, ambapo baadhi ya wadau wa mkutano huo pia wakatoa maoni yao.

Post a Comment