Maduka ya kamari
yameweka dau la kuashiria kuna uwezekano mkubwa wa Harry ane kuondoka
Tottenham na kwenda Manchester United (Daily Star).
Hata hivyo
Tottenham wametupilia mbali uwezekano wa Harry Kane kwenda Old Trafford
na kusema thamani ya mshambuliaji wao ni karibu pauni milioni 200
(Independent).
Alex Sandro, 26, amekubali kujiunga na Chelsea huku
mabingwa hao wa England wakikaribia kukamilisha mkataba wa pauni
milioni 61 kumsajili beki huyo wa Juventus (Corriere della Sera).
Sandro
huenda akaungana na Virgil van Dijk, 25, kutoka Southampton, na
mshambuliaji Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton na kiungo mkabaji wa
Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, wakati Chelsea ikijiandaa kutumia pauni
milioni 240 msimu huu (Daily Express).
Arsenal na Manchester City wanafikiria kubadilishana washambuliaji, Alexis Sanchez, 28, kwa Sergio Aguero, 29 (Daily Star).
Hata
hivyo Alexis Sanchez ameshawishiwa na mchezaji mwenzake wa timu ya
taifa, Arturo Vidal, kwa kuambiwa aachane na Arsenal na kwenda katika
"klabu bora duniani" Bayern Munich (Sun).
Mshambuliaji wa Arsenal
Olivier Giroud, 30, amewasiliana na rais wa Lyon, kabla ya kufanikisha
uhamisho wake kwenda Ufaransa msimu huu (Independent).
Dau la Everton la Pauni milioni 30, la kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, limekataliwa (Mirror).
Chelsea
huenda wakapanda dau la pauni milioni 35 kumtaka beki wa Roma Kostas
Manola, 26, ambaye inasemekana alikuwa anakaribia kuhamia Zenith St
Petersburg ya Urusi (Express).
Meneja wa zamani wa England
Sven-Goran Eriksson amemhakikishia mshambuliaji wa Manchester United
Wayne Rooney, 31, kuwa atapata 'uzoefu mzuri' iwapo ataamua kwenda
kucheza ligi ya China (Daily Mail).
Renato Sanches, 19,
anayenyatiwa na Manchester United amejiweka mbali na taarifa
zinazomhusisha na kuhamia Old Trafford na kusema anatarajia kubakia
Bayern Munich (Record).
Juventus watapanda dau la pauni milioni 15 kumtaka beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares (Sun).
Mshambuliaji
Kylian Mbappe, 19, atapewa ongezeko la mshahara la asilimia 900 na
klabu yake ya Monaco ili kumzuia asiende Real Madrid au Arsenal au
Liverpool zinazomtaka (Sun).
Rais wa Real Madrid Florentino Perez alikutana na familia ya Kylian Mbappe mapema mwezi huu (Telefoot).
Arsenal
na Barcelona zinapigania kutaka kumsajili kinda wa Braga, Pedro Neto,
17, ambaye huenda akawa mchezaji wa miaka 17 aghali zaidi katika
historia ya kandanda, nyuma tu ya Alexandre Pato. Tayari Braga wamekataa
dau la Arsenal la pauni milioni 13.2 (A Bola).
Mshambuliaji wa AC Milan M'Baye Niang ana matumaini
kuwa Arsenal watapanda dau la kumtaka, baada ya kuchelewesha uhamisho
wake wa kwenda Everton (Calciomercato.com).
Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Radja Nainggolan kutoka Roma (Il Tempo).
Liverpool
wanamfuatilia Max Meyer, 21, anayeichezea timu ya taifa ya Ujerumani
chini ya miaka 21 kwenye michuano inayoendelea nchini Poland, lakini
wanakabiliwa na ushindani pia kutoka Tottenham kumsajili kiungo huyo wa
Schalke (Daily Star).
Crystal
palace watamuulizia mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho,
20, ambaye pia anasakwa na West ham, na Leicester (Mirror).
RB
Leipzig hawana mpango wa kumuuza Naby Keita kwa bei yoyote chini ya euro
milioni 80. Liverpool wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa kutoka
Guinea (Bild).
Liverpool wamekataa mkataba wa kubadilishana Faozi
Ghoulam kutoka Napoli kwenda Anfield na Alberto Moreno kwenda Italy
(Liverpool Echo).
Kiungo mchezeshaji wa Real Madrid James
Rodriguez bado anataka kuhamia Manchester United baada ya kukubaliana
maslahi binafsi na Old Trafford (Diario Gol).
Manchester United huenda wakamfuata winga wa
Fiorentina Federico Bernardeshi iwapo watashindwa kumsajili Ivan Perisic
(Football Italia).
Borussia Monchengladbach wanataka kumchukua mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen (Sunday people).
Barcelona huenda wakamgeukia kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez iwapo watashindwa kumpata Marco Verratti (AS).
Meneja
mpya wa Barcelona Ernesto Valverde anataka kupiga hatua ya kushangaza
ya kumtaka kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic (Don Balon).
Bournemouth wanakaribia kukamilisha mkataba wa kudumu wa pauni milioni 20 kumsajili beki wa Chelsea Nathan Ake (The Sun).
Na hatimaye….
Mshambuliaji wa Borussia
Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang alifunga magoli sita akicheza na baba
yake timu moja katika mechi ya kirafiki dhidi ya maveterani wa Paris FC
(tovuti ya Paris FC)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Eid Mubarak!!!! Na Jumatatu njema.
MKUU WA WILAYA YA LIWALE ATOA ZAWADI YA SIKUKUU, kupata habari zaidi bofya >>HAPA
MKUU WA WILAYA YA LIWALE ATOA ZAWADI YA SIKUKUU, kupata habari zaidi bofya >>HAPA
Post a Comment