0



 
US President Donald Trump talks with Secretary of State Rex Tillerson at the White House on 12 June, 2017.
Trump akosa kuandaa chakula cha Eid White House

Rais wa Marekani Donald Trump, amevunja tamaduni ya karibu miaka ishirini kwa kukosa kuandaa chakula cha jioni kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Hafla hiyo inayoandaliwa katika ikulu ya White House imekuwa ikifanyika kila mwaka kutoka kipindi cha Rais Bill Clinton.
Sherehe za Eid al-Fitr ndio mwisho wa mfungo wa Ramadan wakati waislamu hufunga.
Lakini waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson anaripotiwa kukataa ombi la kutaka hafla hiyo kuandaliwa.
Mwezi Mei Reuters ilisema kuwa bwana Tillerson alikataa pendekzeo kutoka kwa idara inayohusika na masuala ya dini ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni kuandaa sherrhe hiyo.


  Former US President Barack Obama hosts the annual Iftar dinner celebrating the Muslim holy month of Ramadan in the East Room of the White House July 22, 2015
Hafla hiyo imeadaliwa na marais watatu akiwemo Rais Barack Obama
Awali Bwana Trump amelaumiwa kwa kutumia maneno makali dhidi ya waislamu ikiwemo kampeni ya kutaka uchunguzi kufanyiwa misikiti nchini Marekani.
Alisema katika taarifa: "Kwa niaba ya watu wa Marekani na Melania ninatuma heri njema kwa waislamu wakati wanaposherehekea Eid al-Fitr.
Chakula cha kwanza cha Eid kilichoandaliwa Ikulu ya White House kiliandaliwa na Rais Thomas Jefferson mwaka 1805 kwa ujumbe kutoka Tunisia.
Sherehe hizo zilifufuliwa tena na Hillary Clinton mwaka 1996 wakati akiwa mama wa kwanza wa taifa.
Hafla hiyo ilianza kufanywa kila mwaka tangu mwaka 1999 na kuhudhuriwa na viongozi wa kiislamu mashuhuri nchini Marekani.



 MKUU WA WILAYA YA LIWALE ATOA ZAWADI YA SIKUKUU, kupata habari zaidi bofya >>HAPA

Post a Comment

 
Top