0
TZ inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi ukanda wa Afrika Mashariki
Image captionTZ inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi ukanda wa Afrika Mashariki
Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la wakimbi la Umoja wa Mataifa UNHCR.
Ripoti hiyo anasema hadi hivi sasa, kuna wakimbizi Laki 2 na elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.
Katika idadi hii kubwa ya watu wanaokimbia nchi yao, UNHCR inasema asilimia 60 ni watoto.
Na ndani ya kipindi cha miezi mitano tu ya mwaka huu wa 2017, wakimbizi 44,487 wamekimbia Burundi na kuingia Tanzania
TZ inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi ukanda wa Afrika MasharikiHaki miliki ya pichaBBC SPORT
Image captionTZ inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi ukanda wa Afrika Mashariki
UNHCR inasema huu ni mzigo mkubwa kwa Tanzania lakini kwa bahati mbaya, nchii hii haipati fedha za kutosha kuwahudumia wakimbizi na wengine wanaotafuta hifadhi
Kambi moja kwa mfano ya Nyarugusu, ambayo inatajwa kuwa ni moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani, inahifadhi wakimbizi 139,0000 idadi ambayo inapaswa kupunguzwa na kuwagawa wakimbizi katika kambi nyingine.
Lakini hili limeshindikana, ripoti ya UNHCR inasema, na ni kwasababu ya kukosekana kwa ardhi ya kufungua kambi mpya
TZ inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi ukanda wa Afrika Mashariki
Image captionTZ inahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi ukanda wa Afrika Mashariki
Hata hivyo serikali ya Tanzania imesifiwa kwa kuendelea kubeba mzigo huu mkubwa wa wakimbizi lakini zaidi kwa kukubali kutekeleza mkakati mpya wa kimataifa ujulikanao kama COMPREHENSIVE REFUGEE RESPONSE.
Mkakati huu kwasasa upo katika hatua za majaribio katika nchi 6 barani Afrika.
Kwa ufupi, huu ni mkakati unalenga kutafuta namna endelevu ya kuwasaidia wakimbizi kupata ulinzi na mahitaji mengine ya msingi ya kibinadamu, lakini zaidi sana kutafuta namna ya kuwashirikisha wakimbizi hawa katika shughuli mbali mbali za maendeleo katika nchi wanazokimbilia.

Post a Comment

 
Top