MKUU
wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amemuweka ndani saa 48 Aliye kuwa
mwenyekiti wa mtaa wa Buguruni kata ya Njombe Mjini halmashauri ya Mji
wa Njombe Emmanuel Ngelime baada ya kutakiwa kuachia madaraka kutokana
na kile kinachodaiwa kuwa amehukumiwa kifungo cha nje kwa miezi 12 na
kutoa maneno machafu kwa mkuu huyo wa wilaya.
Mkuu wa wilaya anasema kuwa sheria inasema kiongozi yeyote akihukumiwa miezi zaidi ya sita anakuwa hana nafasi
ya kuwa katika ofisi ya umma lakini kiongozi huyo alihukumiwa kifungo
cha nje kwa miezi 12 tangu mwaka jana lakini inadaiwa kuwa bado yupo
ofisini.
Akizungunza
nasi mkoani Njombe Msafiri anasema kuwa alifika katika eneo la mtaa huo
kwajili ya kumtaka mwenyekiti huyo Emmanuel Ngelime kuachia ngazi hiyo
lakini alikutana na kauli mbovu na kuagiza askali kumuweka ndani.
Post a Comment