Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliani, Profesa Makame Mbarawa amezindua
rasmi huduma ya kuhama mtandao (MNP) na kuwaonya watoa huduma (mitandao)
watakaowakwamisha wateja wao kuhama.
Profesa
Mbarawa amesema huduma hiyo imeanzishwa ili kumpa uhuru mtumiaji wa
kuchagua huduma bora, jambo litakalowafanya watoa huduma kuboresha
huduma zao.
Amesisitiza
kwamba matumizi ya mfumo wa MNP yatafanikiwa kwa sababu ni rahisi
ukilinganisha na ule wa kuhama kutoka analogi kwenda digitali
uliofanyika miaka michache iliyopita na kuipa sifa Tanzania.
"Tunataka
wananchi wajue kwamba huduma hii ni bure na wasilazimishwe kuhamia
mtandao fulani kwa kushinikizwa. Hii ni Huduma ya hiari na hatutasita
kuchukua hatua kwa kampuni ya simu itakayokiuka utaratibu huu," amesema.
Huduma
hii ya MNP katika Afrika inatumika katika nchi nane, lakini kwa Afrika
Mashariki inapatikana Kenya pekee na Tanzania leo inakuwa ya pili wakati
nchi za Rwanda na Uganda wakiwa kwenye mchakato huo.
Post a Comment