0
El Negro akiwa kwenye makavazi 
El Negro akiwa kwenye makavazi
Katika karne ya 19 lilikuwa jambo la kawaida kwa wazungu kukusanya wanyamapori kutoka sehemu mbali mbali za dunia, na kisha kuwapeleka nyumbani kwao ulaya kuwaweka kwenye makavazi ili waweze kutazamwa.
Hata hivyo raia mmoja wa Ufaransa alivuka mipaka zaidi na kupeleka mwili wa mpiganaji mmoja kutoka Afrika.
Mwandishi mmoja raia wa uholanzi alikumbana na mwili huo ukiwa kwenye makavazi nchini uhispania miaka 30 iliyopita na tangu wakati huo alikuwa na matumaini ya kufuatila asili ya mtu huyo.
Mwili huo ulipata umaarufu kutokana na kusafirishwa kwake na kuwekwa kwa maonyesho ya makavazi kwa kipindi cha miaka 170 nchini Ufaransa na Uhispania.

 Makavazi alimowekwa El Negro
Makavazi alimowekwa El Negro
Je mwili wa El Negro ulitokaje Afrika? Hadithi inaanza wakati Jules Verreaux ambaye ni raia wa Ufaransa, wakati mnamo mwaka 1831 alishuhudia maziko ya mpiganaji mmoja wa jamii ya Tswana barani Afrika.
Jules alifanya mipango ya kurudi usiku ambapo alifukua maiti na kisha kuipa ngozi, gofu la kichwa na mifupa michache.
Akitumia chuma kama uti wa mgongo na mbao kama mabega na magazeti, Jules aliandaa na kutunza sehemu hizo za mwili alizoiba.
Kisha akazisafirisha kwenda mjini Paris pamoja na kreti kadha zilzojaa wanyama. Mwaka 1831 mwili mwa mwafrika huyo uliwekwa kwenye maonyesho ya chumba namba tatu.

  Bustani alikozikwa EL Negro nchini Botswana
Bustani alikozikwa EL Negro nchini Botswana
Gazeti la Le Constitutionel lilimsifu Jules Verreaux ambaye alihatarisha maisha kufanya kitendo kama hicho.
Baada ya zaidi ya nusu karne watu wa Bechuana waliwasili nchini Uhispania.
Licha ya kuwepo upinzani mkalia mambo yalianza kubadilika mwaka 1992, wakati daktari mnoja mhispania aliandika barua ya kutaka El Negro aondolewe kutoka kwa makavazi.
Wito wake uliungwa mkono na watu mashuhuri kama mhubiri Jesse Jackson, mcheza mpira wa vikapu Magic Johnson na Kofi Annan akihudumu kama naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

 Viongozi wa kidini na wanajeshi wakisindikiza mabaki ya EL Negro kwa Maziko
Viongozi wa kidini na wanajeshi wakisindikiza mabaki ya EL Negro kwa Maziko
Lakini kutokana na kuwepo upinzani mkali kutoka kwa watu wa Catalan waliomuenzi EL Negro, ni hadi mwaka 1997 wakati alitoweka kutoka kwa umma. Miaka mitatu baadaye alianza safari ya mwisho kwenda nyumbani.
Mabaki ya mpiganaji huyo wa Tswanma yaliwasilishwa mjini Gaborone ambapo inakadiriwa kuwa watu 10,000 walifika kutoa heshima zao za mwisho
Siku iliyofuatia ya terehe 5 mwezi Oktoba mwaka 2000, alizikwa katika eneo lililowekwa ua katika bustani ya Tsholofelo.

Post a Comment

 
Top