0
Mlipuko mjini New YorkMlipuko mjini New York
Bomu lililolipuka mjini New York lilikuwa tendo la ugaidi ,Gavana Andrew Cuomo amesema, ijapokuwa bado hakuna kundi lolote la kigaidi lilipatikana kuhusika.
Bwana Cuomo amesema kuwa haribifu mkubwa ulisababishwa na bomu hilo na kuongezea kuwa ni bahati kwmaba hakuna mtu aliyefariki.
Bomu hilo la siku ya Jumamosi mjini Man Hatta liliwajeruhi watu 29.
Takriban walinda usalama 1000 wamepelekwa katika maeneo ya uchukuzi mjini humo.
Hakuna mtu ye yote aliyepata majeraha ya kuhatarisha maisha yake.
Polisi wanashuku huenda mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kilipuzi
  Gavan wa New York Andrew Cuomo katikati
Gavan wa New York Andrew Cuomo katikati
Meya wa New York, Bill de Blasio amesema mlipuko huo ulisababishwa kimakusudi lakini akasisitiza kuwa hadi sasa haujahusishwa na kundi lolote la kigaidi.
Amesema pia kuwa hakuna ushahidi kuwa mlipuko huo una uhusiano wowote na bomu la mfereji lililolipuka katika jimbo jirani la New Jersy saa chache zilizopika.
Bomu hilo lililipuka karibu na mahali ambapo mbio za kukusanya pesa za kuwasaidia wanajeshi wa zamani zilikuwa zikiendeshwa.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Post a Comment

 
Top