Maelfu ya maduka katika jimbo la Tamid Nadu nchini India yatasitisha uuzaji wa vinywaji vya Coca-Cola na Pepsi kuanzia Jumatano.
Mashirika
mawili ya biashara yametoa wito kwa washirika wake kususia kuuza
vinywaji vya kigeni na badala yake kukuza bidhaa zinazotengezwa nchini
humo.
Wameshutumu kampuni za vinywaji hivyo kwa kutumia vibaya
maji nchini humo wakati ambapo wakulima wanakabiliwa na hali ngumu ya
ukame.
Hatua hiyo pia inaangazia ushawishi wowote wa kigeni nchini humo.
Shirika
moja linaloshirikisha kampuni za Coke na Pepsi, na shirika la vinywaji
nchini humo limesema kuwa limesikitishwa sana na hatua hiyo.
Post a Comment