0


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi 
Lushoto.Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepiga marufuku uuzwaji wa shamba lenye ekali 455 la Chama cha Ushirika cha Usambara lililoko eneo la Bumbuli wilayani hapa Mkoa wa Tanga.

Lukuvi ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba, mjini Lushoto. Shamba hilo lilikuwa liuzwe ili kurudisha mkopo wa benki wa Sh500 milioni  uliokopwa na chama hicho kwa ajili ya kuendeleza wakulima.

Lukuvi alisema badala ya shamba hilo kuuzwa kwa mtu mwingine, Halmashauri
ya Bumbuli ilichukue na ilipe deni hilo, ili litumike kujenga majengo ya taasisi.

Post a Comment

 
Top