Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akihutubia wananchi baada ya kufungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa
amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi daraja linalounganisha
Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini
Dar es salaam.
Mwandishi wetu
MSTAHIKI MEYA wa Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala, Charles Kuyeko jana alifungua rasmi daraja linalounganisha
Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini
Dar es salaam.
Awali akizungumza katika hafla hiyo
Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku alisema daraja hili
limejengwa kwa takribani mwaka mmoja na kugharimu Tsh.million 478 hadi
kukamilika kwake leo hii. Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku
nyingi kutokana na sababu mbali mbali lakini kutokana na usimamizi imara
wa Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Charles Kuyeko sasa historia
imebadilika.
Meya Kuyeko akizungumza na umati wa
wananchi waliokusanyika kushuhudia ufunguzi huo amewasitiza kulilinda na
kulitunza vyema daraja hilo kwani limejengwa kwa kodi zao.
Awali, Meya akitoa historia ya daraja
hilo amesema kuwa, waliokuwa wanatakiwa kujenga daraja hilo ni wakala wa
Barabara Tanzania (Tanroad) lakini kutokana na kusuasua kwao, Mimi
(Meya) niamua kuingilia kati kwa Manispaa kutenga Fedha kujenga daraja
la muda ili kuwasaidia wananchi wa Bonyokwa kuondokana na atha ya kuwa
Kisiwa hususani wakati wa Mvua.
Kuyeko ambaye pia ni Diwani wa kata ya
bonyokwa amewaambia wananchi hao waliofurika kwenye uzifunguzi huo kuwa
huo ni mwanzo tu wa utekelezaji wa ahadi zake katika kutatua kero za
wananchi na wapiga kura wake. "Nawahakikishia kuwa hamtajutia kunipa
kura zenu kwani daraja hili imekuwa kero ya miaka nenda rudi lakini Mimi
nimeimaliza kwa muda mfupi kwa kushirikiana na watendaji wangu hivyo
mtarajie mengi kabla mwaka huu kuisha hata daladala zitakuwa zinafika
hadi kisiwani".
Mbali na hayo,Meya amewaahidi wananchi
hao muda mfupi ujao atatatua kero ya maji na barabara kama ambavyo
aliahidi kutekeleza wakati wa kampeni.
Ufunguzi huo ulihudhuliwa na viongozi
mbali mbali wa kiserikali na kisiasa akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mhe.
Anatropia Theonest, madiwani wa kata mbalimbali na viongozi wa vyama vya
siasa.
Akitoa salam kwa niaba ya viongozi wa
vyama vya siasa, Dk.Makongoro Milton Mahanga mbunge wa zamani jimbo la
Segerea ambaye kwa sasa ni, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Ilala alisema,
"Tangu niwe kiongozi sijawahi kuona kiongozi mahiri kama Meya Kuyeko.
Ameweza kuwaunganisha viongozi wa
Manispaa yake na kuwa kitu kimoja, na hadi sasa ameshafanya vitu vingi
ambavyo awali vilishindikana nakupongeza sana Meya Kuyeko.
Dkt. Mahanga aliwasisitiza wananchi
kuwaamini viongozi wanaotokana na UKAWA kwani ni wazuri jifunzeni kwa
Kuyeko mambo makubwa anayoyafanya. Kwa niaba ya Chadema nampongeza sana
Meya Kuyeko kwa kukiwakirisha vyema chama kwa wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la
Segerea ndugu Gango Kidera aliwataka wananchi wa Bonyokwa waendelee
kumwamini na kumuunga mkono Meya Kuyeko, Baraza lake la Madiwani kwani
amekuwa mfano bora kwa kutekeleza ahadi zake zinazotokana na ilani na
Sera za Chadema/UKAWA.
Chadema imemtuma Kuyeko kuwatumikia
wananchi wa Bonyokwa na Manispaa nzima ya Ilala kwa kuhakikisha anatatua
kero zao kwa spidi ya mwendokasi na leo tumeona anatenda kwa maslahi ya
wananchi. Nakupongeza sana Meya Kuyeko, alisema Kidera
Viongozi wengine waliozungumza katika
ufunguzi huo ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest ambaye
aliwapongeza wananchi wa Bonyokwa kwa kumchagua Kuyeko, wananchi wa
Bonyokwa mlifanya maamuzi sahihi kuchagua Chadema kwa sababu bila
Chadema Meya Kuyeko tusingempata.
Anatropia pia alimpongeza Meya Kuyeko
kwa kuendelea kutatua kero za wapiga kura wa Bonyokwa siku hadi siku na
Ilala kwa ujumla. UKAWA kwa Manispaa ya Ilala chini ya Meya Kuyeko
imeleta matumaini makubwa kwani wakazi wa Manispaa wapatao 1,415,443
walikuwa wamekata tamaa kabisa kwani viongozi waliopita walishindwa
kutatua kero za wananchi, hivyo UKAWA chini ya Meya Kuyeko ni mfariji
mkuu wa wananchi, alisema Anatropia.
Diwani wa Buguruni Mhe. Penza wa CUF
akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Ilala alisema ilani ya UKAWA
imeweka vipaumbele kwenye Barabara, maji, afya, elimu, na masoko na
mitaji hivi vyote vinafanyika.
Meya Kuyeko aliwashukuru wananchi kwa
kuendelea kumwamini na kumpa ushirikiano wa karibu hali ambayo inampa
ari ya kuwatumikia kwa nguvu zake zote. Pia amekishukuru chama chake
Chadema, viongozi, Madiwani na watendaji wote wa Manispaa ya Ilala
wakiongozwa na Mkurugenzi kwa kumpa ushirikiano wa hali na Mali katika
kuwatumikia wananchi.
Post a Comment