SERIKALI
ya mapinduzi Zanzibar imejidhatiti kuandaa mbinu madhubuti ili kukuza kiwango cha
elimu kitakachopelekea kuongezeka kwa ufaulu katika shule mbali mbali visiwani humo.
Naibu
waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri ametoa kauli
hiyo alipokuwa akizungumza na walimu wakuu, wanakamati wa skuli na masheha wa
wilaya za Magharibi A na B.
Amesema
jitihada zikifanyika kwa wadau wa elimu kuwa na nia ya dhati kuinua kiwango cha
elimu itasaidia kukuza kiwango cha ufaulu nchini.
Pamoja
na hayo amewataka walimu wakuu kuzifahamu na kuzitatua changamoto
zinazowakabili katika skuli zao, hata hivyo amesisitiza walimu kufundisha katika viwango vinavyofaa
na kusomesha kwa wakati hatua aliyoitaja itapunguza kudhorota kwa kiwango cha
elimu Zanzibar.
Post a Comment