MKUU wa wilaya ya
Magahrib A,Visiwani Zanzibar Mwinyi-Ussi Abdallah amezuwia ujenzi wa ukuta eneo la uwanja wa
Garagara
kutokana na kuwepo katika maeneo ya vyanzo vya maji.
Mkuu wa
wilaya amepiga marufuku hiyo alipotembelea eneo hilo, amesema kama ujenzi huo
utaachwa kuendelea unaweza kusababisha madhara kwa siku za baadae.
Amefafanua
kuwa kila mtu anapotaka kujenga anapaswa kuwa na kibali cha ujenzi kutoka
katika mamlaka zinazohusika.
Aidha
mkuu wa wilaya huyo amewatahadharisha wananchi kuwa waangalifu wanaponunuwa
viwanja ili kuepuka kuingia hasara kwa kununua katika sehemu zisizoruhusiwa
ikiwemo kwenye vianzio vya maji.
Post a Comment