IDARA ya usafiri na leseni Zanzibar imeitaka
Serikali kununua mtambo wa kutengeneza beji za madereva na
makondakta kwa lengo la kupunguza udanganyifu wa kughushi beji hizo hali
inayosababishia serikali kukosa mapato.
Hatua
hiyo imetokana na ukaguzi uliofanywa na idara hiyo kwa magari ya daladala na
kubaini idadi kubwa ya beji za kughushi kwa madereva na makondakta wa gari
hizo.
Afisa
usafiri wa idara hiyo Masoud Suleiman ametoa maombi ya mtambo huo alipokuwa
akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa idara hiyo katika kipindi cha robo ya
mwisho ya mwaka 2016 kwa kamati ya
mawasiliano na ujenzi ya baraza la wawakilishi katika ofisi za idara hiyo
Mwanakwerekwe, Mjini Unguja
Nae mwenyekiti wa
kamati hiyo Hamza Hassan Juma ameitaka
idara hiyo kusimamia majukumu ya usalama kwa watumiaji wa barabara kwa
kuendesha shughuli za ukaguzi wa vyombo vya moto, upasishaji wa madereva, kusajili
vyuo vya udereva na uwalimu wa skuli za udereva.
Post a Comment