Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza
Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Magufuli mjini DODOMA.
Kabla ya
Kuongoza Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri, Makamu wa Rais aliwasili leo
asubuhi katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa
Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mndeme, Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga pamoja na
viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan yupo mjini
Dodoma kwa shughuli za kikazi kwa muda wa siku MBILI.
Post a Comment