Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar inakusudia kuimarisha Sekta ya Uvuvi katika azma yake ya kujenga
uchumi imara utakaostawisha maisha ya Wananchi wake.
Akizungumza
na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Uvuvi ya Hong Dong kutoka Nchini China
ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Lan Ping Yong, Ofisini kwake katika jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema
uimarishaji huo utaelekezwa zaidi katika ujenzi wa Viwanda Vidogo vidogo vya
usindikaji wa mazao ya Baharini utakaotoa fursa ya kukaribisha Makampuni na
Taasisi za Kimataifa kuwekeza miradi yao Visiwani Zanzibar.
Balozi
Seif alimuahidi Mkurugenzi Mkuu huyo kuwa pande zinazohusika nchini zitakutana
na kuangalia wazo la Kampuni hiyo la uwekezaji kwa lengo la kuchukuliwa hatua
za muelekeo wa uanzishwaji wa uwekezaji huo.
Mapema
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uvuvi ya Hong Dong ya Nchini China Bwana Lan Ping
Yong amesema mradi wa Uvuvi unaotaka kuwekezwa Visiwani Zanzibar utakuwa na
uwezo wa kutoa fursa za ajira zisizopungua elfu 1,700.
Ameongeza
kuwa Taasisi hiyo imetenga nafasi Tatu kwa ajili ya Watendaji wa Sekta ya Uvuvi
Zanzibar kwenda Nchini Mauritania kujifunza hatua iliyofikia ya Uwekezaji wa
Kampuni hiyo katika Nyanja ya Uvuvi.
Wakati
huo huo Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar amekutana na kufanya mazungumzo na
Balozi mdogo wa India aliyepo Zanzibar Mhe. Barupal.

Post a Comment