Mwenyekiti
wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10.
Manji
alipandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam na kusomewa shtaka la kutumia dawa za kulevya.
Manji
amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa.
Kabla
ya hapo mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Muhimbili
kutokana na matatizo ya moyo yaliyompata baada ya kushikiliwa kwenye kituo
kikuu cha polisi Central.

Post a Comment