0
Waziri wa katiba na sheria Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe amesema sheria ya kumlinda mtoto ya Zanzibar pamoja na ushahidi ni nzuri na itasaidia kupambana na na vitendo vya kijinsia.

        Ametoa pongezi hizo alipokutana na kuzungumza na waziri wa katiba, sheria, utawala bora na utumishi wa umma Zanzibar Haroun  Ali Suleiman huko ofisini kwake mazizini mjini unguja.

Mhe. Mwakyembe amesema  sheria hiyo ipo tofauti na ile ya Tanzania bara,ambapo ameahidi kutumia nafasi hiyo kuangalia baadhi ya mambo kwa lengo la kuirekebishaSheria  kumlinda mtoto ya Tanzania Bara.

Ameongeza kuwa sheria ya ushahidi itasaidia kwa kiasi kikubwa kuona ushahidi unaotolewa na mtoto unakubalika kwa ajili ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Nae waziri wa katiba, sheria, utawala bora na utumishi wa umma Zanzibar Haroun  Ali Suleiman  amesema baraza la wawakilishi limepitisha sheria ya ushahidi ambayo imeboreshwa  zaidi kwa ajili ya kuutambua ushahidi unaotolewa mahakamani na mtoto mdogo.


Aidha ameeleza kuwa baadhi ya wahalifu na mahakimu wamekuwa wakipunguza ushahidi kwa kutumia mwanya hasa pale unapotolewa na wwtoto chini ya miaka 18 pamoja na wenye ulemavu wa akili.

Post a Comment

 
Top