0


Waziri wa biashara, viwanda na masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali amesema Zanzibar itaendelea na mfumo wa ukaguzi wa magari kwa kushirikiana na nchi za kigeni hadi pale yatakapofanyika mabadiliko ili Zanzibar kunufaika zaidi na mapato yanayotokana na ukaguzi huo.

Kwa sasa shirika la viwango Zanzibar ZBC hupata dola 25 kutokana na ukaguzi huo huku dola 125 zikienda katika nchi za kigeni.
 Akitolea ufafanuzi swali la Mwakilishi wa Jang’ombe Abdallah Diwani aliyetaka kufahamu kwanini ZBC inapata pesa kidogo za ukaguzi ikilinganishwa na nchi za kigeni.

Mhe. Balozi Amina amesema licha ya pato hilo kuwa dogo bado Serikali itaendelea kutumia utaratibu huo mpaka pale yatakapofanyika marekebisho.

        Pamoja na hayo waziri huyo amezungumzia vifaa ambavyo tayari vimetumika vinavyoingizwa nchini kuwa hufanyiwa ukaguzi wa kutosha kabla ya kuingizwa nchini.

Post a Comment

 
Top