0


Umoja wa watu wenye ulemavu  Visiwani Zanzibar [UWZ] umeingia ubia na mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF katika mradi wa ujenzi wa nyumba 16 za kupangisha zenye ghorofa nne kwa kila moja.                
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja wa watu wenye ulemavu zanzibar Ali omari makame ofisini kwake kikwajuni mjini Unguja, amesema mradi huo utawasaidia kuwaingizia kipato.
Ameongeza kuwa mradi huo ambao tayari umeridhiwa na Serikali utagharimu  shilingi bilioni 30 mpaka kukamilika kwake.
 Amefafanua kuwa mradi huo utakapokamilika UWZ utakuwa ukipata asilimia 10 ya mapato huku ikikadidiriwa kupata milioni 36 kwa mwaka.
Aidha amesema mradi huo pia utajumuisha ukarabati wa mkubwa wa jengola ofisi ya uwz ili kuwa pahala pazuri na muafaka na pa kufanyia kazi na penye mandhari nzuri..

Post a Comment

 
Top