Mkuu wa mkoa wa mjini
magharib Visiwani Zanzibar Mh Ayoub Muhammed
amewataka wananchi kuwasilisha maoni yao katika taasisi husika juu ya swala
zima la kuanzishwa kwa mpango miji na vijiji Zanzibar.
Akitia
saini ramani ya mpango miji na vijiji pamoja na kuwakabidhi ramani hiyo wakuu
wa wilaya na wakurugenzi wa mabaraza ya manispaa, amesema mpango huo utaongeza
thamani ya ardhi katika mkoa huo na kuwaweka watu wengi katika eneo moja.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa Miji na Vijiji Zanzibar Muhammed
Juma amesema wananchi wamekuwa wakifanya ujenzi holela hali aliyoitaja
kusababisha kizazi kijacho kukosa eneo la kujenga.
Hafla
hiyo imefanyika katika ukumbi wa Rahaleo mjini Unguja.
Kwa mujibu wa takwimu,
mkoa wa mjini magharibi una wakazi laki 5 huku ikikadiriwa kuwa miaka 20 ijayo
mkoa huo utakuwa na wakazi milioni moja na nusu.
Post a Comment