0


BARAZA la manispaa Zanzibar limeahidi kuendelea na zoezi la kukamata ng’ombe na mifugo mengine  katika maeneo ya manispaa ya mji wa Zanzibar linaendelea.


Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni kuripotiwa baadhi ya watu kuanza kurudisha mifugo katika maeneo mbali mbali ya  Manispaa hiyo licha ya kuwepo na marufuku ya kuzuwia mifugo katika Manispaa hiyo.

Mkurugenzi wa baraza la manispaa Zanzibar  Mh Aboud Hassan Serenge amemwambia mwandishi wa blog hii kuwa tangu kuanza kutekelezwa kwa marufuku hiyo, muonekano wa haiba ya manispaa ya mji wa Zanzibar imeimarika.

  Katika hatua nyengine Serenge amesema kuna baadhi ya maeneo ya Manispaa hiyo yalioonekana kupoteza ubora wake kwa sasa mambo yameimarika, huku akitolea mfano  bustani na vipando vya wananchi vinaonekana kustawi.

Post a Comment

 
Top