0


WAKULIMA wa zao la korosho nchini,wametekeleza agizo la Serikali kwa kuotesha na kupanda jumla ya miche mipya 10,396,317,kwa kipindi cha miaka mitatu sasa,ikiwa ni moja ya kuwawezesha kuondokana na umasikini wa kipato.
Kaimu mkurugenzi mkuu,Hassani Jarufu ameyaeleza hayo,alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji,siku ya  uzinduzi wa kampeni ya kupanda mikorosho mipya msimu wa 2016/2017 iliyofanyika kijiji cha Chimbila ‘B’ Tarafa ya Mnacho,wilaya ya Ruangwa,mkoani Lindi,februari 10 mwaka huu.
Taarifa hiyo ilisomwa kwa niaba yake na kaimu mkurugenzi wa Bodi ya korosho,Dustani Kaijage,ilieleza katika kipindi hicho cha kuanzia 2013/14 hadi 2015/16,Serikali kupitia waziri mkuu Kassimu Majaliwa,iliagiza kuoteshwa na kupandwa miche mipya mikorosho 10,000,000 kwa lengo la kuongeza mapato ya mkulima na Taifa.
Kaijage alisema katika kipindi hicho,wakulima kwa kushirikiana na wadau mbalimbali,zikiwemo Halmashauri za wilaya na mikoa inayolima zao hilo hapa nchini,wameweza kupanda na kuotesha miche mipya ya mikorosho 10,396,317 sawa na asilimia 104% na hivyo kuvuka lengo lililokuwa limewekwa.
Akaeleza kwamba katika kipindi hicho,miche 7,641,600 sawa na asilimia 74% ni mikorosho iliyopandwa kwa kutumia mbegu,wakati 2,754,717 sawa na asilimia 26% imepandwa kwa kutumia miche,na kwamba wahusika wanaendelea kutunzwa.
 “Umuhimu wa kupanda miche hii mipya unalenga kuinua uzalishaji bora wa zao la korosho nchini,pamoja kutekleza agizo la waziri mkuu wa Tanzania,Kassimu Majaliwa mwanzoni mwa mwaka jana”Alisema Kaijage.
Kaimu mkurugenzi huyo alisema kutokana na agizo hilo la Serikali, uongozi wa Bodi ya korosho nchini (CBT) iliingia mkataba na vikundi (47) vilivyojishughulisha na uoteshaji mbegu ndani ya mkoa wa Lindi,hivyo kuweza kupata miche 543,327 na kugaiwa kwa wakulima.
“Ni matarajio yetu kuwa ndani miaka (5) hadi (10) ya uteklezaji wa mradi huu,uzalishaji wa korosho utaongezeka na kufikia tani 600,000,hivyo kuongeza mapato yatokanayo na zao hilo”Alisema Kaijage.
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi ambaye alikuwa ndiyo mgeni rasmi katika uzinduzi huo,amewataka wakulima kutokubali kuwa watumwa wa kilimo cha kubahatisha,badala yake waongeze nguvu katika kuzalisha mazao mbalimbali,likiwemo zao la korosho,ili waweze kuondokana na umasikini unaowakabiri.
Pia,Zambi ameiomba Bodi ya korosho kuharakisha upelekaji mapema wa pembejeo,kwa wakulima ili waweze kuzitumia katika kuzalishia mazao,kabla ya msimu haujawapita,sanjari na kuongeza vituo  vitakavyohusika na ugawaji wake,ili kuwaondolea usumbufu wa kufuatilia huduma hiyo mbali na maeneo yao.
”Ninachokiomba kwenu Bodi ongezeni vituo,ili kuwapunguzia wakulima mwendo mrefu wa kwenda Tandahimba kuzifuata hizi pembejeo” Alisema Zambi.
Nae,mwenyekiti wa Bodi hiyo ya korosho Tanzania,Anna Abdallah amelipokea ombi la kiongozi huyo wa mkoa wa Lindi,huku akihaidi kukutana na watendaji wake,ili kulifanyika kazi,huku akiwahasa wakulima kuacha kilimo cha kupanda miti isiyo na faida,badala yake wapande miti ya mikorosho ambayo ina faida

Post a Comment

 
Top