0
Jeshi la polisi Zanzibar limeanzisha uchunguzi wa taarifa za utakatishaji wa fedha kwa watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
              

Kamishna wa polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Bahari Fm ofisini kwake Ziwani mjini Unguja, amesema uchunguzi huo wanaufanya kwa kushirikiana na idara ya usalama wa taifa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP  na mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi Zanzibar ZAECA na taasisi za fedha.

Amefahamisha kuwa, wameanza uchunguzi kwa kuwahoji baadhi ya wanaotuhumiwa pamoja na kuchunguza mfumo wao wa fedha ili kuwagundua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Amefafanua kuwa, uchunguzi huo pia utahusisha maduka ya kubadilishia fedha kutokana na tuhuma fedha nyingi chafu zimekuwa zikipitishwa huko.

Aidha amesema njia hiyo itasaidia kupata kwa kina taarifa na watakaogundulika majina yao yatatajwa hadharani.

Post a Comment

 
Top