0


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Dar es Salaam Young African watashuka Dimbani hii leo  kumenyana na Maji Maji(wanalizombe) katika mwendelezo wa Ligi kuu Tanzania Bara mzunguko ya lala salama



 Katika mchezo wa leo Young African watakuwa wageni katika uwanja wa Maji maji Mjini Songea Mkoani Ruvuma mchezo ambao utapigwa majira ya saa 10:00 za jioni

 
Dar es Salaam Young African leo ikiwa watashinda mchezo wa leo watakuwa wamepunguza gepu la pointi dhidi ya vinara, Simba SC kutoka nne hadi moja.


Simba SC inaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zao 44 baada ya kucheza mechi 18, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 40 za mechi 18 pia.
Dar es Salaam Young African  wamewasili songea jumapili iliyopita  huku wachezaji watano wakikosekana  kwa ruhusa mbali mbali katika kikosi hicho kilichopo songea ikiwemo   beki Vincent Bossou ambaye yuko Gabon na timu yake ya taifa, Togo, mshambuliaji Donald Ngoma na viungo Wazambia Justin Zulu, Obrey Chirwa ambao wote ni majeruhi na Emmanuel Martin aliyekwenda kwenye msiba mkoani Tanga.

Wachezaji wa Young ambao wapo  na Kikosi Mkoani Ruvuma ni  Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa 'Barthez' na Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Pato Ngonyani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan.
Viungo ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Said Juma,  Juma Mahadhi, Deus Kaseke, Simon Msuva, Yussuf Mhilu, Geoffrey Mwashiuya na washambuliaji Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Matheo Anthony. 

Ikumbukwe Young wanashuka katika mchezo huo wakiwa na hasira za kupoteza michezo miwili mfululizo katika michuano ya mapinduzi oikiwemo ule wa kukamilisha makundi katika mchezo wa mwisho wa Kundi B baada ya kupoteza magoli 4-0 dhidi ya Azam na mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali uliowakutanisha na watani zao wa Jadi Simba na kupoteza kwa penart 4-2.




Post a Comment

 
Top