0

YANGA SC imeinyuka Maji Maji ya Songea goli 1-0 na kufikisha point 43 huku wakiendelea kusalia katika nafasi Pili kwa tofauti ya point 1 dhidi ya vinara Simba wenye point 44




Mchezo huo uliopigwa Jioni ya Leo Mkoani Ruvuma katika uwanja wa Maji Maji uliopo mjini Songea ilikuwa ni mwendelezo wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Ushindi huo unawafanya mabingwa hao watetezi, Yanga wafikishe pointi 43 baada ya kucheza mechi 19, ingawa inaendelea kukaa nafasi ya pili nyuma ya vinara Simba SC wenye pointi 44 za mechi 18.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hussein Athumani aliyesaidiwa na Mirambo Tshikungu na Vincent Mlabu, hadi mapumziko Yanga walikuwa tayari mbele kwa bao hilo moja.

Bao hilo lilifungwa na kiungo Deus Kaseke dakika ya 14 kipindi cha Kwanza aliyepiga shuti baada ya kukutana na mpira uliopanguliwa na kipa Agathon Anthony kufuatia krosi ya Nahodha, Haruna Niyonzima.
Baada ya bao hilo, Maji Maji nao wakaanza kushambulia langoni mwa Yanga, lakini safu ya ulinzi ya wana Jangwani ilisimama imara kudhibiti hatari zote.

Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Simba wakiwa wageni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Azam FC wakiwa wenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deogratius Munish 'Dida', Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Oscar Joshua dk90, Amissi Tambwe, Juma Mahadhi na Deus Kaseke/Said Juma ‘Makapu dk’80.
Maji Maji; Agathon Anthony, Salehe Mohammed, Mpoki Mwakinyuke, Keneddy Kipepe, 

Post a Comment

 
Top