Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amefanya uteuzi wa Wabunge wawili
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.
Alhaji Abdallah
Majula Bulembo kushoto ambae jana ameteuliwa kuwa mbunge na hii ni moja ya picha aliyowahi kupiga na Raisi
Magufuli
Wabunge walioteuliwa ni
Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.
Wabunge wateule hawa
wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.
Kituo cha kazi na
tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa
baadaye.
Post a Comment