Serikali ya mapinduzi Zanzibar
imepongezwa kutokana na kasi kubwa inayoionesha katika kuboresha miundombinu huku ikuungwa mkono na mataifa na
taassisi washirika wa maendeleo Duniani.
Makamu wapili wa raisi Zanzibar Baloz Seif Aly Iddi (kulia)akizungumza na Balozi wa korea nchini Tanzania
Balozi wa
Korea kusini nchini Tanzania Song Geum Yong ameyasema hayo wakati
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga
Mjini Zanzibar aliyekuwepo Visiwani Zanzibar katika uzinduzi wa Skuli ya
Sekondari ya Kwarara pamoja na kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za kutimia
miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema
Taasisi na Makampuni ya Korea yanafurahia mabadiliko hayo na kuamua
kusaidia ujenzi wa Miradi ya Kielimu akiutolea mfano ujenzi wa skuli hiyo uliomalizika
hivi karibuni ili kuipa nguvu zaidi Sekta ya Elimu Zanzibar
ambayo ndio kichwa cha maendeleo hayo.
Amefahamisha
kuwa, anapata faraja kuona ujenzi wa Skuli hiyo uliopata msaada kutoka
Shirika la Maendeleo ya Korea KOICA, Good Neighbors, Shirika la Utangazaji la
Korea SBS na Taasisi ya Wasanifu Majengo ya Korea umekwenda sambamba na ujenzi
wa Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Tumaini.
Akitoa
shukrani zake kwa misaada mbali mbali inayotolewa na Korea kwa Tanzania Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amesema Korea ya Kusini
inastahiki kupongezwa kwa jitihada zake za kuunga mkono maendeleo ya
Zanzibar, lakini hata hivyo alimshauri Balozi Song kutumia maarifa
yake katika kuzishawishi Taasisi na Makampuni ya nchi yake kuendelea kuelekeza
nguvu zao katika uwekezaji wa sekta tofauti ikiwemo ile ya usafiri wa
Baharini.
Amesema
sekta ya Kilimo Zanzibar hasa katika upande wa umwagiliaji pia inastahiki
kuungwa mkono zaidi ili kuwaongezea nguvu za uzalishaji Wakulima kwa vile
zaidi ya asilima 80 ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar wanaendesha maisha yao
kwa kutegemea sekta hiyo.
Post a Comment