Naibu Katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi CCM
Tanzania Bara, Rodrik Mpogolo ameungana na zaidi ya vijana 400 wa UVCCM kutoka
katika mikoa mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara katika uzinduzi wa
matembezi ya kuadhimisha miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumza
katika uzinduzi huo katika viwanja vya Donge Kijibweni mkoa wa Kaskazini
Unguja, Mpogolo amewataka vijana wa chama hicho kuendelea kujiimarisha na kuwa
tayari kukabiliana na jaribio lolote la kuhatarisha Mapinduzi ya Zanzibar
ya Mwaka 1964.
Amesema endapo vijana
hao watatumia nguvu na uwezo walionao katika kulinda, kusimamia na kupigania
mapinduzi hayo vizazi vijavyo vitaweza kurithi nchi ikiwa katika mikono salama.
Mpogolo amewasihi
vijana hao kuendeleza dhana ya uzalendo katika kusimamia maslahi ya Chama na
Serikali zote mbili kama walivyofanya vijana wa zamani ambao ni waasisi wa
Mapinduzi hayo.
Viongozi mbali mbali wa
Chama na Serikali wamehudhuria uzinduzi huo wakiwemo Mwenyekiti wa Mkoa wa
Mjini Borafya Silima Juma, Mwenyekiti wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhani Ali
Kichupa, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Issa Juma, makatibu na Wenyeviti wa Wilaya, Majimbo na
Matawi.
Matembezi hayo ya siku
tatu yaliyoandalia na UVCCM, hufanyika kila mwaka, kauli mbiu ya
mwaka huu ni asiyeyaenzi
mapinduzi ya Zanzibar ni adui
wa maendeleo ya Zanzibar.
Post a Comment