Wakati Zanzibar ikielekea
kuadhimisha miaka 53 ya mapinduzi wiki ijayo, Waziri wa katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora Haroun Ali Suleiman
amempongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt. Ali
Mohamed Shein kwa kuonesha nia ya dhati kuboresha maslahi kwa watumishi wa
umma.
Akizungumza liwale blog ofisini kwake Mazizini, mjini Unguja Mhe. Haroun amesema hatua hiyo
itasaidia kuinua maisha ya watumishi hao kwani kima cha chini cha mshahara
kinatarajiwa kupanda kutoka shilingi laki moja na nusu hadi laki 3 mwezi Aprili
mwaka huu.
Pia
ameeleza kufurahishwa na hatua ya Mhe. Rais kuanzisha tume ya maadili ya
viongozi wa utumishi wa umma ambapo ameitaja tume hiyo kuwa itasaidia katika
vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.
Pamoja
na hayo Mhe. Haroun amesema wizara yake imejitahidi kupambana na vitendo vya rushwa kwa kuanzisha kitengo cha rushwa na kutumia mbinu kadhaa.
Post a Comment