Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi amesema kukamilika kwa miradi tofauti iliyoanzishwa na
Serikali chini ya mradi wa huduma za jamii mijini itasaidia kuondosha ama
kupunguza mafuriko ambayo huwakumba wananchi katika msimu wa mvua kila mwaka.
Makamu wa Pili a Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ukuta wa
kuzuia maji ya Bahari
Balozi
Seif ameeleza hayo wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa
Ukuta wa Ukingo wa Bahari hapo Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar ikiwa
ni miongoni mwa harakati za shamra shamra za kusherehekea miaka 53 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar.
Amesema
mafanikio ya mradi huo tayari yameanza kuonekana katika ujenzi wa michirizi ya
maji ya mvua kwenye maeneo ya Daraja Bovu, Mnazi Mmoja, Kijangwani na baadhi ya
maeneo ya Jang’ombe na Wananchi wake tayari wanafaidika na matunda ya
mradi huo.
Amesema
Serikali ya Mapinduzi imejipanga kuimarisha miradi hiyo ikiwa sehemu ya
Jududi za utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 ikilenga
kuwaondoshea usumbufu unaowakumbwa wananchi walio wengi hasa wale wa maeneo ya
Ng’ambo ya Mji.
Ujenzi wa
Ukuta wa Ukingo wa Bahari hapo Mizingani Forodhani Mjini Zanzibar
unasimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kupitia Mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya shilingi Bilioni 7 kutoka Benki
ya Dunia.
Post a Comment