Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema Serekali imeandaa mikakati
madhubuti kuhakikisha kunakuwa na uchumi endelevu pamoja na kuzitambua rasilimali
na biashara za wanyonge zinazomilikiwa kinyume na utaratibu wa kisheria.
Ametoa kauli hiyo wakati wa
uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mkurabita Shehia ya Kiungoni Wilaya
ya Wete, Kaskazini Pemba ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya miaka 53 ya
mapindunzi ya Zanzibar na kuwataka wananchi hao kulitumia vyema jengo hilo.
Amesema kuwa wajibu wa
Serekali na Mkurabita ni kuwawezesha wananchi kupata hati za kumiliki
ardhi kwa ajili ya kuzitumia na kukuza mitaji yao. Hivyo wananchi
wametakiwa kuukubali mpango huo ili wapate maendeleo .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati
ya Mkurubita John Chiligati amewataka wafanyabiashara wadogo wadogo kuchukua
leseni na kusajili biashara zao ili waweze kunufaika kwa kupata mitaji na
kukuza biashara zao kupitia mikopo kutoka vyombo mbali mbali.
Shilingi million 62 laki 8 na
96 elfu zimetumika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo.
Post a Comment