0
Na Mwandishi Wetu

Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam AZAM FC maarufu kama wanalamba lamba  imemaliza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B Kombe la Mapinduzi ikiwa  kileleni baada ya kuifunga Yanga mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa jana, usiku katika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Matokeo hayo yanaifanya timu ya Azam iwe katika nafasi ya kwanza  kwa pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja, huku yanga ikiwa nafasi ya pili na point sita ikiwa imecheza mechi tatu na kushinda mbili na kufungwa moja

kwa matokeo hayo  Azam itacheza na mshindi wa pili wa Kundi A katika Nusu Fainali, wakati Yanga itacheza na mshindi wa kwanza wa kundi hilo .
Hadi mapumziko, Azam walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco, Adebayor.

Bocco alifunga bao hilo dakika ya pili tu kwa shuti kali baada ya kuukuta mpira uliopanguliwa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ baada ya shuti kali lililopigwa na  kiungo Joseph Maundi.   
Baada ya bao hilo, Yanga walijaribu kufunguka kwa kuongeza mashambulizi, lakini safu ya ulinzi ya Azam iliyoongozwa na mabeki Aggrey Morris na Yakubu Mohammed ilionekana kuwa imara masaa yote
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika  Yanga walikuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa katika dakika ya 2 na JOHN Rafael BOKO.


Kipindi cha pili nyota ya Azam  walipata mabao matatu kupitia kwa Mshambuliaji Mghana, Yahya Mohammed dakika ya 54,Mahundi akafunga bao katika  dakika ya 80 na Winga Mghana, Enock Atta Agyei aliyetokea benchi akaifungia Azam bao la nne dakika ya 85.
Kiujumla Dar es Saalam haikucheza katika kiwango kizuri kama wanachama na wapenzi wa club hiyo walivyotarajia na kama Azam ingetumia nafasi walizozipata vizuri huenda wangepata idadi kub way a mabao.
 
kikosi cha Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji/Geoffrey Mwashiuya dk73, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan, Justin Zulu/Said Juma ‘Makapu’ dk61, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko/Deus Kaseke dk83 na Juma Mahadhi/Emmanuel Martin dk34.

Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed/Abdallah Kheri dk91, Stephan Mpondo, Joseph Mahundi, Frank Domayo/Enock Atta Agyei dk79, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Mudathir Yahya dk86 na Yahya Mohammed/Samuel Afful dk65.

Post a Comment

 
Top