WANANCHI
mjini Njombe wameilalamikia halmashauri ya Mji huo kuto pita kwa wakati
kuondoa taka walizo kusanya tayari katika viroba kama ilivyo kawaida ya
halmashauri hiyo kupitisha gari na kusababisha taka kutupwa maeneo
mbalimbali ya barabara za mji.
Wamesema
kuwa halmashauri awakli ilikuwa ikipitisha gari kwa wakati lakini kwa
sasa gari haipiti kwa wakati na kusababisha baadhi ya wakati hao kukaa
na taka kwa muda mrefu majumbani kwao.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakazi hawa wanaomba halmashauri kuboresha mifumo
ya uzoaji wa taka ama kurejesha vizimba kwa kuwa wapo tayari kulipia
huduma ya kupitiwa na gari ya taka.
Halmashauri
inasema kuwa iliweka mdhabuni kwaajili ya kuondoa taka mtaani lakini
kuna matatizo kidogo na mdhabini huyo na amesimamishwa kwa muda wakati
wapo kwenye mazungumzo.
Kwa
upande wake mdhabuni anasema kuwa amesimamishwa kwa muda na halmashauri
wakati wapo kwenye mazingumzo lakini pia fedha kutoka halmashauri
zimekuwa zikichelewa ndio maana wamekuwa wakisuasua.
Halmashauri
ya mji Njombe ilifanya utaratibu wa kuondoa taka mtaani kwa kufuta
vizimba na huduma hiyo ilianza mwezi Julai na kuanza kusuasua mwezi
novemba mwishoni kutokana na matatizo hayo lakini wakati huduma inaanza
iliboresha usafi wa mazingira mjini.
Post a Comment