0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto imetenga bilioni 251 ili kuimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na zahanati zote nchini .
Hayo yamesemwa na  Katibu Mkuu Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa mahojiano katika kipindi cha Tunatekeleza kinachoendeshwa na kituo cha matangazo TBC1 jijini Dar es salaam.
“Kutokana na taarifa zinazozagaa juu ya upungufu wa dawa katika zahanati hapa nchini ,taarifa hizo si za kweli napenda kuwatoa hofu wananchi na bajeti yetu ya mwaka huu ni shilingi Bil.  251 kwa ajili ya dawa tu,” alisema Dkt. Ulisubisya.
Katibu Mkuu Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya alisisitiza kuwa kuna dawa zitapewa kipaumbele kutokana na mahitaji yake kuwa makubwa nchini ukilinganisha na mahitaji ya dawa nyingine hivyo dawa zote zitaendelea kuwepo ili kuwasaidia wananchi wote wenye uhitaji.
Dkt. Ulisubisya aliweka wazi juu ya mipango ya serikali katika kuimarisha huduma za afya katika maeneo mbali mbali nchini ili kujenga taifa lenye watu imara kiafya.
Kwa mujibu wa Dkt. Ulisubisya amesema kuwa  vituo vya serikali na vya watu binafsi ni vyema viendelea kufuata sera, taratibu na sheria ikiwemo bei elekezi katika kuwahudumia wananchi huduma bora kwa gharama ndogo.
Dkt. Ulisubisya amesisitiza kuwa Kufikia mwezi wa tano mwaka huu asilimia 90 ya dawa zote zitakua zimepatikana na kusambazwa kwenye vituo vya afya na zahanati zote nchini ili kuimarisha sekta ya afya na mpaka sasa chanjo zote zipo za kutosha.
“Tunataka kila kituo cha afya kinachojengwa sasa hivi kitoe huduma za upasuaji ili kupunguza mlundikano  wa wagonjwa wanahoitaji huduma hiyo na kuokoa maisha ya mtanzania kwa haraka zaidi,” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya alisema kuwa Serikali ina mkakati wa  kuimarisha huduma zote za vipimo ili zipatikane katika hospitali za wilaya na kikanda mpaka kufikia 2020 ili kuwezesha taifa kupiga hatua katika sekta ya afya.

Post a Comment

 
Top