Upinzani nchini Burundi wafahamisha kuomba mpatanishi mpya kunako mzozo wa Burundi ambao kwa sasa unaelekea mwaka wa pili.
Vyama vya upinzani katika umoja wa CNARED wamefahamisha kuwa mpatanishi
Benjamin Mkapa ameonesha upande anaoegamia jambo ambalo ni kinyume na
wadhifa aliopewa wa upatanishi.
Upinzani huo umemuomba rais wa Uganda Yoweri Museveni kumteua mpatanishi mpya ili kupatia suluhu mzozo wa Burundi.
Kwa upande mwingine CNARED imeomba ushirikiano wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kutoa msaada wao kwa mpatanishi mpya.
CNARED iligoma kumtambua Benjamin Mkapa baada ya kufanya ziara nchini
Burundi Disemba 30 na kusema kuwa muhula wa 3 wa rais Nkurunziza ni haki
yake kikatiba.
Watu zaidi ya 700 wamefariki tangu rais Nkurunziza kuteuliwa kuwania kiti cha urais Aprili 2015.
Vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi vikidai kuwa ni kinyume na
mkataba wa Arusha uliokomesha vita vya tangu mwaka 1993 hadi mwaka 2006.
Post a Comment