Katika kuhakikisha
malengo ya Serikali ya kuwa na uchumi wa kati yanafikiwa, taasisi zinazopokea
malalamiko ya wananchi zimetakiwa kuyafanyia kazi kwa kuwapatia majibu na
kuchukua hatua dhidi ya malalamiko hayo.
Rai hiyo imetolewa na Afisa elimu kutoka idara ya haki za
binadamu, Rukia Fadhil alipokuwa akitoa mada kwenye mafunzo ya siku mbili
kuhusu haki za binadamu na utawala bora yaliyofanyika kwenye ukumbi wa kituo
cha huduma za sheria Zanzibar Kijangwani mjini Unguja.
Amesema ili kuhakikisha uwajibikaji unaongezeka nchini ni
vyema Serikali ikasisitiza utekelezaji wa kusimamia mikataba ya huduma kwa
wateja.
Amefafanua kuwa suala la uwajibikaji lina nafasi kubwa katika
kuleta utawala bora na kukuza uchumi wa nchi na linapaswa kutekelezwa na viongozi
pamoja wananchi.
Kwa mujibu wa utafiti mdogo uliofanywa na idara ya utawala
bora Zanzibar kwa watendaji wa Serikali na baadhi ya taasisi zisizo za Serikali
hali ya uwajibikaji nchini sio ya kuridhisha asilimia 38.79 ya wafanyakazi
wanatekeleza majukumu yao kwa wastani.
Utafiti huo umefanywa kwa wafanyakazi 165.
Post a Comment