Mwenyekiiti wa
Chama cha ADC)Hamad Rashid Mohamed amesema si kweli kama Katibu Mkuu wa
CCM Abdulrahman Kinana hajui kinachoendelea katika sakata la
uchaguzi Mkuu Zanzibar ila katibu huyo wa CUF Maalim Seif Sharif
Hamad amekwama kisiasa na kuamua kuwadangaya wafuasi wake.
Mwenyekiiti
wa Chama cha ADC)Hamad Rashid Mohamed
Amesema mazumgumzo
yoyote ya kusaka aidha upatanishi au usuluhishi wa kisiasa Zanzibar kwanza
hupata baraka toka vyama vya siasa huku makatibu wakuu wote
wakifahamu na kushiriki katika vikao vya kamati za pamoja.
Mh:Hamad ametoa
matamshi hayo leo katika viwanja vya Komba Wapya alipozindua Barabara ya Bizred iliyopo Mkoa wa mjini Magharibi katika shamrashamra za
kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema njia
za kusaka mazumgumzo ya upatajishi wa kisiasa au hitilafu ya
kisiasa katika nchi yoyote aghalab hutumika njia tatu kuu ili
kupata muafaka au makubaliano .
Amezitaja njia
zenyewe kuwa ni serikali na chama tawala cha nchi husika kikubali kama kuna
tatizo , jumuiya ya kimataifa na watendaji wakee waombe kuingilia kama kweli
vipo viashiria vya tatizo lenyewe ili kufanya mazumgumzo na tatu ikiwa ni
kufanya Mapinduzi na si vinginevyo.
Katika hatua
nyengine mh Hamad alisema haiwezekani
kuwepo na mazumgumzo ya kusaka mapatano huku Rais aliyeshinda yuko madarakani,
aondoshwe ili apishwe mwingine kushika madaraka wakati hukutangazwa na Tume ya
uchaguzi kama mshindi halali kwa mujibu wa katiba na sheria.
Hata hivyo
kiongozi huyo wa ADC aliwataka wazanzibari kuendelea kuishi katika maisha ya
maelewano, ili waweze kuendeleza amani iliyopo hapa nchini
Post a Comment