Mgombea ubunge kupitia
tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Juma Ali Juma katika uchaguzi mdogo jimbo la
Dimani ameahidi kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake ndani ya
jimbo hilo kwa kutafuta mtaalamu kuendesha mafunzo ya ujasiriamali.
Mgombea
Ubunge Wa Jimbo La Dimani Kwa Tiketi Ya Ccm Juma Ali Juma (wapili toka kulia) katika uchaguzi mdogo wa jimbo la dimani
Akizungumza na Liwale Blog mgombea huyo amesema mafunzo hayo
ya yatakayodumu kwa miezi mitatu itahusisha utengenezaji wa sabuni ya maji,
sabuni ya mche na sabuni ya maji ambapo hayo yote ameahidi kuyafanya punde
baada ya kuingia madarakani.
Juma
amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kufanya kila mmoja awe na uwezo wa
kujiajiri wenyewe bila ya kuitegemea serikali na hatumae wanayanyuka kimaisha
Katika hatua nyengine Juma Aly amewasihi wananchi wa jimbo la
Dimani kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura ifikapo Januari 22
ili kutimiza haki yao ya msingi na kukichagua chama cha mapinduzi katika
uchaguzi huo.
Post a Comment