ASKOFU Mkuu
wa Makanisa ya Anglikana Tanzania Mhashamu Dk. Jacobe Chimeledya
amemstaafisha kwa lazima Askofu Valentino Mokiwa kwa tuhuma za kuhusika
na matumizi mabaya ya madaraka na mali za kanisa.
Askofu Mokiwa hadi anastaafishwa alikuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu
wa barua kwa mapadri na maoskofu wote wa Kanisa la Anglikana Jimbo la
Dar es Salaam ambayo MTANZANIA inayo nakala iliyoeleza sababu za
kufukuzwa kwake kuanzia juzi Januari 7, mwaka huu na kwamba sio tena
askofu wa makanisa hayo.
Akizungumza
na MTANZANIA kwa simu jana Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi iliyoundwa
kwa ajili ya kumchunguza Mokiwa, Sylivester Haule alisema kiongozi huyo
alilazimishwa kuvuliwa uaskofu huo ambapo awali alikaidi.
Haule ambaye
pia ni Mkuu wa Kanisa la Mtakatifu Andrea lililopo Magomeni Jijini Dar
es Salaam, alithibitisha kuvuliwa kwa uaskofu wa Valentino Mokiwa.
Alisema
sababu za kuvuliwa madaraka kwa kiongozi huyo wa muda mrefu wa kanisa
hilo ni kudaiwa kuhusika kwake na ufujaji wa mali za kanisa na matumizi
mabaya ya madaraka.
Alisema
hatua hiyo inatokana na mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake na
wadhamini wa makanisa mbalimbali ya jimbo la Dar es Salaam, ambayo ni
Yombo Buza na Magomeni ambayo walilalamikia hatua ya matumizi mabaya ya
madaraka kwa kile walichoita ufisadi huku wakimtaka aandike barua
mwenyewe ya kujiuzulu lakini aligoma kufanya hivyo.
Alisema
Mokiwa alikuwa akikabiliwa na mashtaka 10 ambapo shtaka la tatu la
uwekezaji ndiyo lililomtia hatiani na yeye kukiri kosa mbele ya tume
hiyo ya uchunguzi.
“Katika
shtaka namba tatu lilikuwa ni pamoja na kufuja mali za kanisa ikiwa ni
pamoja na ekari 400 zilizopo kanisa la Buza alimega ekari 200 na kumpa
mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Kishimba huku kanisa likiwa halina
taarifa.
“Pi a
wadhamini walimlalamikia lakini hakuweza kusikia huku akiendelea kuuza
na kugawa mali zingine za kanisa kinyemela kinyume na makubaliano ya
vikao na utaratibu wa kanisa,” alisema Haule
Mwenyekiti
huyo wa Tume ya Uchunguzi, alisema kuwa eneo lingine ambalo liliingia
katika kosa namba tatu ni la Benki ya Wanachi Dar es Salaam (DCB),
ambayo makubaliano ya awali wawekezaji hao walitakiwa kufanya ujenzi
kulipa Sh bilioni 5 kisha kuwa mali ya Kanisa lakini Mokiwa aliandikisha
kwa Sh bilioni mbili na baada ya mkataba kuisha Mokiwa aliwatetea
wawekezaji hao.
“Unajua
ilikuwa ni kama aina fulani ya ufisadi maana makubaliano na waliojenga
ilikuwa walipe Shilingi bilioni tano walivyotugeuka Askofu Mokiwa
anatetea naye na kusema kuwa ni Shilingi bilioni mbili jambo ambalo si
sahihi,’’ alisema
“Baada ya
yote hayo kubainika Askofu Mokiwa hakukanusha alikiri makosa lakini
alitakiwa kujiondoa yeye mwenyewe kwa kuandika barua ya kujiuzulu siku
ya Desemba 7, mwaka jana ila alikaidi pia huku akiendelea na kazi zake
mpaka hapo alipovuliwa kwa lazima,’’alisema Haule.
Aliongeza
kuwa baada ya kukaidi maaskofu wakuu walikutana kwa ajili ya kujadili
suala hilo kuanzia Desemba 21 hadi 24 na baada ya hapo maamuzi
yakatolewa Januari 7 kwa kuamua kuwa si Askofu tena.
Aliongeza kuwa Askoafu Mokiwa kwa sasa anatakiwa kukabidhi ofisi za kanisa na kufanyiwa ukaguzi wa hesabu.
Mwandishi
alipomtafuta Askofu Mokiwa ili kuzungumzia taarifa za kuvuliwa kwake
madaraka, simu yake ya mkononi haikupatikana na juhudi za kumtafuta
zinaendelea.
Na Asha Bani
Chanzo : Mtanzania
Post a Comment