Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, leo amewateua Mabalozi watano
kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja Mabalozi walioteuliwa na
vituo vyao vya kazi kama ifuatavyo;
Balozi Mbelwa Brighton
Kairuki ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Beijing – China.
Balozi George Kahema
Madafa ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Rome – Italy.
Balozi Emmanuel John
Nchimbi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Brasilia – Brazil.
Balozi Fatma M. Rajab
ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Doha- Qatar.
Balozi Prof. Elizabeth
Kiondo ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Ankara – Uturuki.
Balozi Dkt. James Alex
Msekela ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania Geneva – Umoja wa Mataifa.
Shughuli ya kuapishwa
mabalozi hao itafanyika kesho saa 10:30 Jioni Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amemteua Muhidin Mboweto kuwa
Balozi.
Tarehe ya kuapishwa na
kituo cha kazi cha Mboweto kitatangazwa baadae.
Post a Comment