0


Simba ya Dar es salaam imeshindwa kufanya vema katika uwanja wa nyumbani baada ya kufungwa bao moja kwa sifuri na matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam fc mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa Taifa Jijin Dar es Salaam
            


Mchezo huo ligi kuu Tanzania Bara umepigwa majira ya saa 10:00 za jioni ya leo ambapo nahodha John Raphael Bocco  ndie alieipatia tumu yake ya Azam ushindi baada ya kushinda goli hilo katika dakika 70 ya mchezo.

Bocco alifunga bao hilo baada ya kupata mpira kutoka kwa mshambuliaji Mghana Mohammed Yahya na kumchenga beki wa kati wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali na kupiga shuti dogo lililomshinda  kipa Mghana, Daniel Agyei. 

baada yah ii leo samba kupoteza mchezo sasa inakuwa ni  kipigo cha pili mfululizo ndani ya mwezi mmoja Simba wanapewa na Azam, baada ya Januari 13 kufungwa pia 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar, bao pekee la Himid Mao. 


Kipigo hicho kinapunguza matumaini ya ubingwa kwa Simba SC, iliyouanza vizuri msimu, kwani ikibaki na pointi zake 45 za baada ya kucheza mechi 20 inaweza kuenguliwa kileleni na Yanga ikiifunga Mwadui Uwanja wa Taifa.

Makocha wote Mcameroon Joseph Marius Omog na Mromania Aristica Cioaba walianzisha mshambuliaji mmoja mmoja katika vikosi vyao, upande wa Azam Nahodha John Bocco na Simba, Juma Luizio.
Kulikuwa na viungo wengi kwa timu zote, upande wa Azam wakianzishwa, Mcameroon Stephan Kingue, Himid Mao, Joseph Mahundi, Frank Domayo na Ramadhani Singano ‘Messi’ na Simba wakianzishwa Jonas Mkude, Said Ndemla, Jamal Mnyate, Muzamil Yassin na Pastory Athanas.
Hata hivyo, ilikuwa ni bahati yao Azam FC baada ya kosa kosa za pande zote mbili kwa muda mrefu, Nahodha Bocco akafunga dakika ya 70.
Bocco mwenye bahati ya kufunga dhidi ya vigogo Simba na Yanga, alifunga bao hilo pekee dakika ya 70.
Baada ya kuruhusu bao hilo, Simba wakafunguka zaidi kusaka bao la kusawazisha kwa kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam.
Lakini safu ya ulinzi ya Azam ikiongozwa na ‘beki mbabe’, Aggrey Morris ilisimama imara kudhibiti mashambulizi yote ya Simba.
Kikodi cha Simba SC leo kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu/Ibrahim Hajib dk59, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Said Ndemla, Jamal Mnyate/Shiza Kichuya dk47, Muzamil Yassin, Pastory Athanas na Juma Luizio/Laudit Mavugo dk65.
Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue/Mudathir Yahya dk77, Himid Mao, Joseph Mahundi, Frank Domayo, John Bocco/Abdallah Kheri dk83 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Yahya Mohammed dk63.

Post a Comment

 
Top