WAJUMBE wa
Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wameeleza
kushangazwa kushindwa kufanya kazi miradi mikubwa kutokana na kukosekana kwa
umeme.
Mweyekiti wa Kamati
hiyo Mhe. Hamza Hassan Juma ametoa kauli hiyo kutokana na uwanja wa Ndege
kisiwani Pemba kwa baadhi ya kazi kusimama kutokana na kukosekana kwa umeme wa
uhakika.
Amesisitiza kuwa
haiwezekani kwa Serikali, wizara zinazohusika na uongozi wa uwanja huo
kushindwa kutafuta transfoma maalum uwanjani hapo ili kuruhusu miradi mikubwa
iliyopo iweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumzia
suala hilo, Naibu Waziri wa ujenzi mawasiliano, na usafirishai Zanzibar
Mohameda Ahmad ametoa rai kwa viongozi wa uwanja huo kujenga utamaduni kukutana
na viongozi husika ili kutatua changanmoto zinazowakumba na sio kufanya mambo
kienyeji enyeji.
Post a Comment